Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uruguay kushughulikia kesi za walinda usalama wake

Uruguay kushughulikia kesi za walinda usalama wake

Ujumbe kutoka nchini Uruguay umewasili nchini Haiti ili kuchunguza madai kuwa wanajeshi wake wa kulinda amani walio kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Haiti walihusika kwenye vitendo vya dhuluma za kingono. Hata hivyo msemaji wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Haiti (MINUSTAH) Eliane Nabaa anasema kuwa ikiwa madai hayo yatapatikana kuwa ya ukweli Umoja wa Mataifa una mipango ya kuwaunga mkono wahusika kwa njia za kisheria, kiafya na kisaikolojia. Walinda usalama hao kwa sasa wanazuiliwa kwenye kambi za Uruguay huku kamanda wao akiachishwa kazi.