Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila kujua kusoma na kuandika hakuna maendeleo:UM

Bila kujua kusoma na kuandika hakuna maendeleo:UM

Wiki hii dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika, takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu zaidi ya milioni 700 duniani na hasa watu wazima hawajui kusoma na kuandika.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limesema bila kufuta ujinga kwa kujua kusoma na kuandika ambayo ni haki ya binadamu, basi maendeleo yatasalia kuwa ndoto katika jamii nyingi.

Matatizo ya kutojua kusoma na kuandika yapo zaidi katika nchi zinazoendelea na hususani kwenye maeneo ya vijijini. Nini sababu? na je hatua zipi zinachukuliwa kuhakikisha hali hii inatokomezwa na ujinga kufutwa kabisa?.

Mwandishi wetu wa Nairobi Kenya Jason Nyakundi amedodosa hali halisi ya elimu nchini humo ambapo kwa sasa walimu wako katika mgomo wa kitaifa na kutuandalia makala hii.

(MAKALA NA JASON NYAKUNDI)