IOM yagharamia filamu inayoainisha changamoto za uhamiaji Afrika Kusini

9 Septemba 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limepiga jeki mpango wa utengenezaji wa filamu maalumu ambayo inashabaa ya kuanisha changamoto na hali ngumu kwenye uhamiaji.

Ofisi ya shirika hilo nchini Afrika Kusini ambayo ndiyo imegharamia utengenezaji wa filamu hiyo imesema kuwa masuala mengine yaliyopewa uzito ni juu ya maisha ya ugenini, hali ya shaka  inayowaandama wahamiaji pamoja na utambulisho wa kitaifa.

Filamu hiyo imepewa jina la “ Man on Ground” Pamoja na kupigwa jeki na IOM pia makundi ya watu mbalimbali na mashirika ya kibiashara yamesaidia kugharimia filamu hiyo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter