Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi ya kujitoa mhanga nchini Pakistan

Ban alaani mashambulizi ya kujitoa mhanga nchini Pakistan

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataiafa Ban Ki- moon amelaani vikali mashambulizi ya kujitoa mhanga yanayowalenga maafisa wa ngazi za juu jeshini nchini Pakistan ambayo yamewaua watu kadha na kuwajeruhi wengine wengi.

Kwenye habari iliyotolewa na msemaji wake Ban alionyesha kuhuzunika kutokana na kuendelea kuuawa kwa watu wengi nchini Pakistan kupitia kwa njia za kigaidi. Hata hivyo Ban amepongeza jitihada za serikali ya Pakistan za kukabiliana na ugaidi akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa unaunga mkono wananchi wa Pakistan kwenye jitihada hizo.