Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uangalizi mzuri wa ardhi utasaidia kuzuia moto wa asili msituni:FAO

Uangalizi mzuri wa ardhi utasaidia kuzuia moto wa asili msituni:FAO

Nchi zimetakiwa kutoa kipaumbele katika kukabiliana na moto katika maeneo yanayopakana na misitu ili kuzuia asilimia 95 ya moto wa msituni ambao huzuka kutokana na shughuli zinazofanywa na binadamu kwenye misitu hiyo.

Onyo hilo limetolewa na mpango wa kimataifa wa ushirikiano wa misitu CPF ambao unajumuisha mashirika 14 ya kimataifa na sekretarieti. Na umetoa kauli hiyo kufuatia mataifa mengi kukabiliwa na ongezeko la moto katika misitu yao kwa kutokuwa na mipango mizuri ya kudhibiti moto.

George Njogopa anaripoti.