Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 70 wameuawa katika machafuko ya kikabila na kidini Nigeria

Watu 70 wameuawa katika machafuko ya kikabila na kidini Nigeria

Watu takriban 70 wameuawa katika machafuko ya kikabila na kidini kwenye jimbo la katikati mwa Nigeria la Belt tangu kuanza kwa mwezi Agosti imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu.

Ghasia zinafanyika hasa katika mji wa Jos ambako kuna mashambulizi kati ya vijana wa Kiislam na Kikristo. Rupert Colville ni msemaji katika ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema pia anatiwa hofu na shughuli za kundi lijulikanalo kama Boko Haram ambalo limedai kuhusika na mashambulizi ya bomu ya karibuni kwenye jengo la Umoja wa mataifa mjini Abuja.