Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali bado ni tete kwenye jimbo la Blue Nile Sudan:UNHCR

Hali bado ni tete kwenye jimbo la Blue Nile Sudan:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema hali ya usalama bado ni tete kwenye jimbo la Blue Nile nchini Sudan na kusababisha maelfu ya watu kukimbilia katika nchi jirani ya Ethiopia.

Hali imetokana na kuzuka kwa mapigano baina ya majeshi ya serikali ya Sudan na wafuasi wa Sudan Peoples Liberation Movement (SPLM) wiki moja iliyopita.

Watu zaidi ya 4004 wamesemekana kuvuka mpaka na kuingia mashariki mwa Ethiopia kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR Fatoumata Lejeune -Kaba .

(SAUTI YA FATOUMATA KABA)