Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafungwa watoroka jela kusini mashariki mwa DRC

Wafungwa watoroka jela kusini mashariki mwa DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MONUSCO unaelezea wasi wasi uliopo kuhusu usalama wa magereza kwenye taifa hilo la DRC baada ya tukio ambapo wafungwa walitoroka jela kwenye eneo moja la kusini mashariki mwa nchi.

Zaidi ya wafungwa 960 akiwemo Gedeon Myungu Mutanga aliyekuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Mai Mai walikimbia jela baada ya watu waliokuwa wamejihami kulivamia jela hilo lililo kwenye vitongozi vya mji wa Lubumbashi. Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa wafungwa 150 kati yao washakamatwa lakini hata hivyo bwana Mutanga bado hajatiwa mbaroni. Mutanga anakabiwa na hukumu ya kifo baaada ya kuhukumiwa na mahakama ya kijeshi mwaka 2009.