Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yaitaka Interpol kutoa kibali cha kukamatwa Gaddafi

ICC yaitaka Interpol kutoa kibali cha kukamatwa Gaddafi

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Luis Moreno Ocampo ameiomba shirika la kimataifa la polisi INTERPOL kutoa tangazo la kukamatwa kwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi kwa madai ya kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu, kwa mauaji na ukatili.

Ocampo ameongeza kuwa kukamatwa kwa Gaddafi ni suala la muda. Tangazo la INTERPOL la kukamatwa kwa awali huwa ni la watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwasafirisha au kuwasalimisha kwa mahakama ya kimataifa kulingana na kibali cha kukamatwa kilichotolewa au uamzi wa mahakama.

Ocampo pia ameomba INTERPOL kutoa tangazo la kukamatwa Saif Al-Islam Gaddafi na Abdullah Al-Senussi. Ameongeza kuwa ofisi yake inaendelea na uchunguzi kuhusu Libya na kwamba kuna uhalifu ambao hautofumbiwa macho na jumuiya ya kimataifa.