Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Australia yapongezwa kwa kuchangia vikosi vya kulinda amani:Ban

Australia yapongezwa kwa kuchangia vikosi vya kulinda amani:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipongeza Australia kama nchi ya kwanza kuchangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa. Ban aliyekuwa akizungumza na wanafunzi katika chuo kikuu cha Sydney amewashukuru pia watu wote wa Australia kwa kuusaidia kumaliza mvutano katika kanda hiyo ikiwemo Timor Mashariki, Boganinville na visiwa ya Solomon.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Australia imekuwa ni nguvu muhimu katika masuala mengi yanayotusumbua kwa sasa, kukabiliana na umasikini wa kimataifa, kuchagiza kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, kupigia upatu upokonyaji silaha na kuwa na dunia huru bila silaha za nyuklia.

Katika hotuba yake amegusia pia hali inayoendelea nchini Syria na kusema Rais Assad ameshindwa kutimiza ahadi alizotoa. Amewataka vijana kuwa na msimamo na fikra pana, watumie ari waliyonayo kuleta mabadiliko na kushirikia  mambo makubwa kuliko fikra zao binafsi kwa manufaa ya  taifa nzima.