Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Syria hajatimiza ahadi yake:Ban

Rais wa Syria hajatimiza ahadi yake:Ban

Rais wa Syria Bashar al-Assad hajatimiza ahadi ya kusitisha matumizi ya nguvu dhidi ya wanaoandamana kwa amani amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Ban amesema jumuiya ya kimataifa inahitaji kuwa na kuali moja kuhusu suala la Syria wakati ambapo waandamanaji wanaendelea kukabiliwa na matumizi ya nguvu na ghasia.

Akizungumza ziarani New Zealand Ban amesema amemuomba Rais Assad mara nyingi kusitisha matumizi ya nguvu dhidi ya raia. Ameongeza kuwa pia amemuomba rais Assad kutekeleza mabadiliko ya kisiasa aliyoahidi. Ban amesema kwa bahati mbaya ahadi hizo hajatimiza na jumuiya ya kimataifa imeshindwa kuchukua mtazamo wa pamoja kama ilivyofanya kwa Libya na Ivory Coast.