Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Syprus na Uturuki wajadili masuala ya mali:UM

Viongozi wa Syprus na Uturuki wajadili masuala ya mali:UM

Viongozi kutoka jamii ya Cypriot nchini Uturuki na wale kutoka nchini Ugiriki wamefanya mkutano wao wa kwanza unaoangazia masuala ya umiliki wa mali kwenye mazungumzo yanayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa ya kukiunganisha kisiwa hicho cha Mediterranean ambacho kimegawanyika kwa karibu miaka 50.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Cyprus Alexander Downer aliwaambia waandishi wa habari kufuatia mkutano kati ya rais Dimitris Christofias na rais Dervis Eroglu kuwa mkutano ulifanyika katika mazingira mema huku kila upande ukijitahidi kuafikia makubaliano.

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa yaling’oa nanga mwaka 2008 kwa lengo kubuni serikali iliyo na kiongozi mmoja na yenye majimbo yaliyo yenye hadhi sawa.