Walinda amani wa UM kuondolewa nchini Haiti

7 Septemba 2011

Wanajeshi watano wa Uruguay wanaofanya kazi na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Haiti MINUSTAH wamekamatwa kwa madai ya kulawiti kijana wa Kihaiti mwenye umri wa miaka 18.

Tukio hilo limebainika hadharani baada ya video ya kitendo hicho ambacho ni kinyumbe na misingi ya Umoja wa Mataifa kuonekana kwenye mtandao. MINUSTAH ina wanajeshi 9000 kwenye kisiwa hicho cha Caribean vikiwemo vikosi kutoka Uruguay. Kamanda wa vikosi vya MINUSTAH ni Meja Jenerali Luiz Ramos.

(SAUTI YA MAJOR LUIZ RAMOS)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter