Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM, Lebanon wajadili hali ya vikosi vya kulinda amani

UM, Lebanon wajadili hali ya vikosi vya kulinda amani

Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wamekuwa na majadiliano ya ana kwa ana na Waziri Mkuu wa Lebanon katika jitihada za kuimarisha majukumu ya ulinzi wa amani katika eneo hilo. Pande zote mbili yaani Umoja wa Mataifa na Waziri Mkuu Najib Mikati zimejadilia juu ya nafasi ya vikosi vya kulinda amani vilivyopo nchini humo, ambayo vimeongezewa muda wa kusalia huko kwa miezi mingine 12.

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani kwenye eneo hilo Alberto Asarta amesema kuwa hatua iliyochukuliwa na baraza la usalama kuongeza muda wa vikosi hivyo kusalia huko ni hatua muhimu ambayo pia imezingatia mashirikiano mema baina ya jeshi la taifa la Lebanon. Lebanon imetajwa kuwa na dola ya kupigiwa mfano kutokana nanma inavyosukuma mbele ustawi wa wananchi wake.