Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufisadi ni uhalifu na kikwazo cha maendeleo:UM

Ufisadi ni uhalifu na kikwazo cha maendeleo:UM

Ufisadi umetajwa kama uhalifu unaoathiri nchi nyingi na jamii kote duniani, unaovuruga ukuaji wa uchumi, maendeleo , demokrasia, haki ya kisheria na pia haki za binadamu.

Kati ya masuala yanayochangia kuwepo kwa ufisadi ni pamoja na kuwepo mbinu dhaifu za kupambana na ufisadi pamoja na ukosefu au kutopata habari zinazostahili.

Wizara inayohusika na masuala ya uwazi na vita dhidi ya ufisadi nchini Bolivia imeungana na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC ili kutoa hamasisho dhidi ya ufisadi.

Moja ya kampeni zitakazotolewa inalenga kuwafunza watu kuhusu masuala yanayohusiana na ufisadi huku sehemu ya pili yenye kichwa kugundua uhalifu ina lengo la kutoa hamasisho kuhusu jinsi uhalifu unavyoshikamana na ufisadi.