Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Puntland, Galmudug zaafiki kushirikiana

Puntland, Galmudug zaafiki kushirikiana

Viongozi wanaotoka katika majimbo ya Galmudug na lile la Puntland yaliyoko nchini Somalia wamehaidi kuweka shabaya ya pamoja ya kuendeleza mashirikiano kukabiliana na vitisho zinavyoibuka kwenye eneo hilo. Kwenye kikao cha pamoja kilichofanyika mjini Mogadishu kujadilia ukomo wa serikali ya mpito wa Somalia , maraia wa majimbo hayo Mohamed Ahmed Alin, na Abdirahman Mohamed Mohamud wametiliana saini makubaliano yanayohimiza mawasiliano mema baina ya pande zote ili kutanzua mkwamo unazuka kwenye eneo hilo.

Tukio la utiaji saini makubaliano hayo ambayo inatajwa kuwa ni muhimu kwa ustawi wa eneo hilo, imeshuhudiwa pia na spika wa bunge la mpito Sheikh Adan, na mawaziri kadhaa walioko kwenye serikali ya mpito. Akizungumza kandoni mwa mkutano huo unaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, mwakilishi wa Katibu Mkuu kwenye eneo hilo Augustine Mahiga amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa inaashiria mwanzo mzuri.