Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua mwanadiplomasia wa Ufaransa kuwa mkuu wa vikosi vya kulinda amani

Ban amteua mwanadiplomasia wa Ufaransa kuwa mkuu wa vikosi vya kulinda amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameteua mwanadiplomasia wa kifaransa Hervé Ladsous kuwa mkuu mpya wa shughuli za ulinzi wa amani akiwajibika kusimamia zaidi ya watumishi 100,000 wanaofanya kazi za kulinda amani duniani kote.

Mwanadiplomasia ameteuliwa kushuka wadhifa huo baada ya mtangulizi wake Alain Le Roy kujiuzulu mapema mwezi uliopita.

Bwana Ladsous ni mwanadiplomasia wa muda mrefu na amaozuefu mkubwa na masuala ya mahusiano ya kimataifa.

Kabla kuwa ya kuwa balozi wa Ufaransa nchini China, alipata kufanya kazi katika wizara ya mambo ya nje ya nchi yake kama mkuu wa utumishi.

Pia anatajwa kuwa ni mtu mwenye weledi mkubwa na masuala ya siasa na utawala. Pia amepata kufanya kazi za kidiplomasia katika nchi za Marekani,Australia, Switzerland, na Indonesia.