Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

jumuiya ya kimataifa yatakiwa kuunga mkono mkataba kupinga majaribio ya nyuklia

jumuiya ya kimataifa yatakiwa kuunga mkono mkataba kupinga majaribio ya nyuklia

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa na Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Josef Deiss kuhakikisha utekelezaji wa mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia.

Wito huo umekuja wakati baraza la Umoja wa Mataifa lilipofanya kikao maalumu Ijumaa kuadhimisha siku ya kimataifa dhidi ya majaribio ya nyuklia siku ambayo huadhimishwa rasmi Agost 29.

Bwana Deiss ameipongeza Kazakhstan ambayo kimsingi ilipiga marufuku majaribio ya nyuklia miaka 20 iliyopita kwa kujukua jukumu la kuongoza kampeni ya kutokomeza majaribio ya nyuklia.

Amesema kwamba mkataba maalumu wa kupinga majaribio ya nyuklia (CTBT) ambao ulipitishwa mwaka 1996 kwa bahati mbaya bado haujaanza kutekelezwa.

(SAUTI YA JOSEF DEISS)

Mkataba wa sasa wa kimataifa kupinga majaribio ya nyuklia ambao unaheshimiwa karibu na mataifa yote sio mbadala wa kutekeleza kwa kina wajibu ulioko kwenye CTBT. Hivyo naitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua juhudi zote zinazohitajika kuridhia mkataba wa kimataifa na na kufuatilia kwa kila hali uidhinishwaji wake ili utekelezwe kikamilifu.”

Ingawa mataifa 154 yametia saini na kuridhia mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia, mataifa tisa zaidi ambayo mengi yna silaha za nyuklia yanahitaji kuridhia mkataba huo kabla haujaanzwa kutekelezwa. Mataifa haya ni Marekani, Uchina, India, Pakistan, Korea Kaskazini, Israel, misri, Iran na Indonesia.