Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano mkuu kuandaliwa Somalia

Mkutano mkuu kuandaliwa Somalia

Mkutano wa hali ya juu wa kumaliza kipindi cha mpito nchini Somalia utaandaliwa mjini Mogadishu kuanzia tarehe 4 hadi 6 mwezi huu. Mkutano huo ulio wa aina yake na wa kwanza kuandaliwa mjini Mogadishu kwa miaka mingi unatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu wajibu muhimu kwa serikali ya Somali na bunge.

Mkutano huo utawajumuisha wawakilishi kutoka kwa serikali ya mpito, bunge la serikali ya mpito, Puntland, Galmudug na Ahlu Sunna Wal Jama’a.