Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR atembelea pembe ya Afrika wakati wa Eid

Mkuu wa UNHCR atembelea pembe ya Afrika wakati wa Eid

Mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR António Guterres amesema kuwa wafanyikazi wa kutoa misaada nchini Somalia wanakabiliwa na wakati mgumu wakati wanapojaribu kuwasaidia karibu watu 400,000 waliohama makwao waliopiga kambi ndani na nje ya mji mkuu Mogadishu.

Guterres alitembelea pembe ya Afrika juma hili kuonyesha uzalendo kwa wasomali waliohama makawao wakati wa sherehe za Eid il-Fitr wakati wa kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan. Akiwa ziarani humo Wasomali wanaoshi kwenye sehemu kama Maajo walimweleza mkuu huyo wa UNHCR kuhusu maisha yao ya kila siku. Faith Kasina afisa wa UNHCR anayesafiri na Guterres alizungumza na Radio ya UM kuhusu ziara hiyo.
(SAUTI YA FAITH KASINA)