Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aipongeza mahakama ya Bolivia kwa kuwahukumu waliohusika kwenye uhalifu

Pillay aipongeza mahakama ya Bolivia kwa kuwahukumu waliohusika kwenye uhalifu

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha uamuzi wa kihistoria wa mahakama nchini Bolivia ya kuwahukumu waliokuwa mawaziri wawili na maafisa wa ngazi za juu jeshini kwa kuhusika kwenye vifo vya zaidi ya watu 60 wakati wa maandamano ya kuipinga seikali yaliyofanyika mwaka 2003 na kuutaja uamuzi huo kama njia bora ya kumaliza ukwepaji wa sheria.

Katika kile kijulikanacho kama “Black October” watu 69 waliuawa na zaidi ya wengine 400 kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga mpango wa serikali wa kujenga bomba la gesi katika eneo la El Alto karibu na La Paz.

[George Njogopa na taarifa kamili.]