UM walaani kitendo cha UK kutaka kuwatimua wahamiaji walioko kwenye mashamba ya Dale

2 Septemba 2011

Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa inayojishughulisha na upigaji vita vitendo vya ubaguzi wa kirangi imelaani vikali hatua inayochukuliwa na Mamlaka ya Uingereza ambayo inapanga kuwaondosha familia ya wahamiaji walioko kwenye mashamba ya Dale, ikisema kuwa kitendo hicho ni sawa na kuziendea kinyume haki za binadamu.

Uingereza imegoma kuyatii malalamiko toka jumuiya ya kimataifa ikisisitiza kuwa itawahamisha wahamiaji hao na haijawa tayari kuwaandalia mazingira ya kule wanakofikia.

Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa hatua hiyo inaweza kuleta taswira mbaya kwa wahamiaji hao na inahofia makundi ya watoto na wanawake uwezekano wa kutumbukia kweny6e dhiki na shida kubwa. Imeitaka Uingereza kulegeza kamba na wakati huo huo kuangalia njia nyingine mujarabu ambazo hazitaweza kuwaathiri jamii hiyo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud