Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova alaani dhuluma dhidi ya waandishi wa habari nchini Syria

Bokova alaani dhuluma dhidi ya waandishi wa habari nchini Syria

 

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea uhuru wa vyombo vya habari amelaani dhuluma zinazoendelea kuendeshwa dhidi ya waandishi wa habari nchini Syria na kuutaka utawala wa nchi hiyo kuheshimu haki za binadamu ikiwemo haki ya kujieleza. Matamshi hayo ya Irina Bokova ambaye ni mkurugezi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO yanajiri baada ya ripoti za kutisha kutoka nchini humo.

Karibu raia 2000 wa Syria wameuawa kwa muda wa miezi mitano iliyopita tangu yalipoanza maandamano ya kuipinga serikali sawia na maandamano yaliyoshuhudiwa kwenye maeneo ya Afrika Kaskazini na mashariki ya kati yaliyosababisha mapinduzi kwa seikali za muda mrefu.