Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR aizuru Mogadishu, aomba misaada zaidi

Mkuu wa UNHCR aizuru Mogadishu, aomba misaada zaidi

Mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR António Guterres ameishauri jamii ya kimataifa kuongeza misaada kwa watu waliohama makwao nchini Somalia. Akiongea alipofanya ziara ya kwanza kabisa kuwai kufanywa na mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa tangu miaka ya tisini Guterres amesema kuwa jamii ya kimataifa inastahili kufanya bidii kuwafikia watu popote walipo nchini Somalia.

Kwa muda kwa miezi miwili iliyopita zaidi ya Wasomali 100,000 wengi wakiwa ni wakulima wafugaji wamekimbilia mji mkuu Mogadishu kutoka maeneo yanayokumbwa na ukame ya Bay, Bakool na Lower Shabelle.

Faith Kasina ni afisa wa UNHCR  Somalia asema.