Mahakama ya ICC yakataa ombi la Kenya la kutaka kutupiliwa mbali kesi

31 Agosti 2011

Mahakama ya kimataiga kuhusu uhalifu wa kivita ICC imetupilia mbali wito wa serikali ya Kenya wa kutaka kutupiliwa mbali kwa kesi zinazowakabili maafisa sita wa ngazi za juu serikalini zinaohusiana na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Sita hao ni pamoja na naibu waziri mkuu Uhuru Muigai Kenyatta, wabunge William Samoei Ruto na Henry Kiprono Kosgey , mwandishi wa habari Joshua Sang, Mkuu wa Utumishi wa Umma Francis Kirimi Muthaura na aliyekuwa kamishna wa polisi Mohamed Hussein Ali. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

Zaidi ya watu 1,100 waliuawa, 3,500 wakajeruhiwa na hadi wengine 600,000 walazimika kuhama makwao kufuata ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa Disemba mwaka 2007. Pia kuna madai ya kuendeshwa ubakaji na uharibifu wa mali nyingi kwenye mikoa sita kati ya mikoa minane nchini Kenya. Mahakama hiyo ilisema kuwa haikufanya makosa yoyote baada ya kugundua kuwa serikali ya Kenya ilishindwa kutoa ushahididi wa kutosha wa kubaini kuwa ilikuwa ikiwachunguza washukiwa hao sita kuhusiana na kesi zilizo mbele ya mahakama ya ICC. M

apema mwaka huu Katibu Mkuu wa UM Ban Ki Moon alijadiliana na makamu wa rais wa Kenya Kalonzo Musyoka kuhusu kesi hizo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud