Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulizi nchini Nigeria halitavuruga shughuli za UM: Migiro

Shambulizi nchini Nigeria halitavuruga shughuli za UM: Migiro

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha–Rose Migiro amesema kuwa shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya makao makuu ya Umoja wa

Mataifa kwenye mji mkuu wa Nigeria Abuja juma liilopita haliwezi kuuzuia Umoja wa Matifa katika kuendeleza shughuli zake nchini humo. Bi Migiro aliyatamka haya mara baada ya kurejea kutoka nchini humo alikokwenda kushuhudia athari za shambulizi hilo. Bi Migiro anasema kuwa alishtushwa aliposkia kuhusu shambulizi hilo na alizungumza na Ben Marlor wa Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu alichoshuhudia.