Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro wa kibiashara kati ya Kosovo na Serbia

Mgogoro wa kibiashara kati ya Kosovo na Serbia

Mvutano uliosababishwa na mgogoro wa kibiashara kati ya Kosovo na Serbia unaendelea. Kaimu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo, Farid Zarif amelieleza Baraza la Usalama kwenye  mkutano hii leo.

Amesema Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyopelekwa mbele ya  Baraza la Usalama inaonyesha mawasaliliano mazuri kati ya Kosovo na Serbia wakati wa muda wa ripoti uliomalizika tarehe 15 Julai.

“Baada ya hapo hali ilibadilika, kuanza na kuhairishwa kwa kikao cha sita cha mazungumzo ya Pristina-Belgrade kutokana na kutoelewana kati ya vyama kuhusu suala la mihuri ya Forodha ya Kosovo. Tarehe 20 Julai, Pristina ilitangaza kuanzishwa  hatua ya “kubadilishana vipimo” kwenye bidhaa za Serbia kwa kuviwekea vikwazo”.

Kosovo ilijitenga kutoka Serbia mwaka 2008 na kutangaza uhuru lakini bado mamlaka ya Serbia inajadili ukweli wa uhuru huo.