UM wataka mataifa yote duniani kukomesha “ Uhalifu wa kupindukia”

30 Agosti 2011

Umoja wa Mataifa umetoa zingatia la kuyataka mataifa yote duniani kuachana na kile ilichokiita “ uhalifu wa kupindukia”kwa kuendesha mwenendo wa chini chini kuwaangamiza watu waliokimnbia uhamishoni kwa shabaya ya kupata hifadhi mpya katika nchi ngeni.

Alice Kariuki  na taarifa kamili .

Umoja huo wa mataifa umesema kuwa baadhi ya dola duniani zinaendesha fagio la kuwatowesha kimya kimya watu hao ambao wamekimbia nchi zao za asili kwa sababu ya vita ama mkwamo mweingine wa kijamii. Katika taarifa yao ya pamoja timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa inayoaangazia hali hiyo imesema kuwa katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, familia nyingi zilizokimbia uhamishono zimejikuta zikitumbukia kwenye matukio hayo ya kinyama.

Timu hiyo ya wataalamu ambayo taarifa yake  imetolewa katika kilele cha kuadhimishwa siku ya kimataifa juu ya waathirika na vitendo hivyo, imataja unyama mwingine kuwa ule unaojulikana kama wa muda mfupi kwa wahusika kuwatorosha waathirika hao na kuwaficha kwa kipindi kufupi na baadaye hutekeleza dhamira zao. Imesisitiza juu haya ya kukomeshwa kwa mwenendo huo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud