Mkuu wa UNHCR aenda kula Eid pembe ya Afrika

30 Agosti 2011

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi António Guterres yuko katika ziara eneo la pembe ya Afrika kuungana na wananchi wa eneo hilo kusherekea sikukuu ya Eid El Fitr. Kamishna huyo amechukua fursa hiyo kukutana na wananchi walioko kwenye mazingira magumu kuonyesha uungaji mkono wake hasa katika kipindi hiki cha kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa ramadhani.

Akiwa huko anatazamiwa kusambaza misaada mbalimbali ikiwemo ile ya chakula kwa mamia ya Wasomalia. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud