Wahisani wengine wawasaidia waathirika wa mapigano ya kikabila Sudan Kusini:IOM

30 Agosti 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limefanikiwa kusambaza huduma mbalimbali za kijamii kwa mamia ya raia wa Sudan Kusini ambao waliondoka kwenye maskani zao na kwenda uhamishoni kutokana na hali mbaya ya usalama katika jimbo la Jonglei.

Ikisaidiana na Jamhuri ya Sudan Kusini, shirika hilo la umoja wa mataifa limesambaza vifaa vinavyojumuisha vyandarua 5,000 kwa ajili ya kukabiliana na mbu waenezao malaria. Vifaa vingine ni mablanketi 5,000 na msaada wa vifaa vya vyakula vinavyofikia 3,500.

Wakazi wa eneo hilo la Jonglei waliingia kwenye mapigano ya kikabili na kusababisha watu zaidi ya 600 kupoteza maisha na wengine kadhaa wakijeruhiwa katika kile kilichoelezwa ugomvi wa mifugo.  Maafisa wa serikali wanasema kuwa zaidi ya watu 250,000 wameashwa bila makazi kufuatia ugomvi huo uliohusisha makabila ya Murle na Nuer.

Masharika ya kimataifa yanaona kuwa makundi maalumu kama wanawake na watoto wanasalia kwenye shida kubwa ya kukosa nyumba za kuishi hasa katima msimu huu wa mvua.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud