UM washtushwa juu ya mauwaji ya kutisha yaliyofanyika Libya

30 Agosti 2011

Umoja wa Mataifa umesemwa kuwa umeshtushwa juu ya ripoti zinazosema kuwepo kwa mauwaji ya mamia ya watu pamoja na vitendo vya ukandamizwaji wa haki za binadamu matukio yanayodaiwa kufanyika nchini Libya. Uhalifu huo kwa kiasi kikubwa unadaiwa kufanywa na vikosi vitiifu kwa utawala wa Gaddafi licha kwamba ripoti nyingine zinavitaja vikosi vya waasi kuwa ni sehemu ya matukio hayo.

Hali ya wasiwasi pia imezidi kujitokeza kufuatia kutojulikana waliko wafungwa kadhaa ambao walitiwa gerezani wakati wa utawala wa Gaddafi kabla na baada ya machafuko kuanza. Kamishna ya haki za binadamu imevitaka vikosi vitiifu kwa Gaddafi kufichua kule waliko wafungwa hao kabla maisha yao hayajapotezwa.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud