Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu kujadili shambulizi la bomu kwenye majengo ya UM Abuja

Baraza kuu kujadili shambulizi la bomu kwenye majengo ya UM Abuja

Watu waliofariki dunia kwenye shambulizi la bomu lililolenga ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Abuja, Nigeria sasa wameongezeka na kufikia 23. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, idadi hiyo ya vifo inajumuisha watumishi 10 wa Umoja huo ambao ni raia wa Nigeria na mmoja raia wa Norway.

Watu wengine nane waliouwawa walikuwa sio wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wengine watatu bado hawajatambulika uraia wao. Katika shambulizi hilo la bumo, watu 826 wameripotiwa kujeruhiwa.

Baraza Kuu la Umoja  wa Mataifa linatazamiwa kukutana kwa mkutano maalumu kujadilia hali hiyo. Tayari Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Asha-Rose Migiro amerejea  New York kutoka Abuja alikoenda kujionea hali jumla ya mambo.