Hatua ya Darfur kuwapa msamaha wafungwa yapongezwa na UNAMID

29 Agosti 2011

Muungano wa vikosi vya kulinda amani vya kimataifa katika jimbo la Darfur nchini Sudan vimetoa taarifa ya kuonyesha kuridhishwa kwao kufuatia mamlaka ya nchi hiyo kuwaruhusu masheik kadhaa waliokuwa wakipata hifadhi kwenye maskani ya vikosi hivyo wakihofia usalama wa maisha yao kurejea kwenye maskani zao.

Masheikh hao wapatao 5 walilazimika kuomba hifadhi kwenye majengo ya vikosi hivyo ambavyo vinaundwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID kwa kuhofia usalama wa maisha yao.

Wameishi kwenye eneo hilo wakipatiwa hifadhi kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa hofu kwamba wangetiwa mbaroni kutokana na kudaiwa kuhusika kwao kwenye machafuko yaliyozuka mwaka uliopita wa 2010. Gavana wa jimbo la Sudan Kusini ametoa msamaha huo kwa masheikh hao kama sehemu ya kusherekea sikukuu ya Eid al-Fitr ambayo inahitimisha mfungo wa mwezi wa ramadhani.

Monica Morara na taarifa kamili

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud