Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kusambaza maji Tripoli

UNICEF kusambaza maji Tripoli

 

Shirika la kuhudumia watoto UNICEF leo linatazamiwa kutoa chumba za maji zinazofikia 90,000 mjini Tripoli ikiwa ni nyongeza ya chumba nyingine 90,000 zilizotolewa hapo kabla.

Hatua hiyo inalenga kukabili mkwamo wa ukosekanaji wa maji ambao unaiandama maeneo mbalimbali ya Libya hasa mji mkuu wa Tripoli. Hadi sasa kiasi cha lita milioni 5 za maji kimewasili nchini humo kutoka katika nchi za jirani. Mkuu wa UNICEF nchini humo Christian Balslev-Olesen amesema kuwa wasaidizi wake kwa hivi sasa wanafanya kazi pamoja na maafisa wa Libya ili kuratibu hatua hiyo ya utoaji wa maji ya dharura.