Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya wajadiliwa

26 Agosti 2011

Ban amejadili hali nchini Libya kupitia video na viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu, Shirika la Ushirikano wa Kiislamu, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa wote walioshiriki katika majadiliano haya pamoja na serikali ya mpito wamesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika kuisaidia Libya kutekeleza mipango yake baada ya vita akiongeza kuwa ombi la kwanza la Walibya ni kwenye upande wa misaada ya dharura, hasa afya na matibabu.

(SAUTI YA BAN)

Katibu Mkuu ameupongeza uamuzi wa Baraza la Usalama alhamisi kuachilia dola bilioni 1.5 zilizohifadhiwa. Amesisitiza kuwa katika wakati huu muhimu jamii ya kimataifa ina wajibu wa kuungana ili kuhakisha wakati wa mpito katika nchi hiyo ya Afrika Kaskakazini utaendelea bila matatizo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter