Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili operesheni za kulinda amani

Baraza la usalama lajadili operesheni za kulinda amani

 

Watendaji wote wanaoshiriki katika oparesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa wanapaswa kutoa maoni yao na kusikilizwa wakati maamuzi yanafanyika juu ya mamlaka ya kulinda amani. Hii ni kulingana na taarifa ya Baraza ya Usalama iliyotolewa kwenye mkutano hii leo kujadili hali ya operasheni za kulinda amani.

Taarifa hiyo inathibitisha kuwa chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ni wajibu wa Baraza la Usalama kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Balozi Hardeep Singh Puri kutoka India ambaye ni Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa Agosti asema.

(SAUTI TA HARDEEP SINGH PURI)

Kabla ya kuanza mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu operesheni za kulinda amani, wajumbe wa baraza hilo walikuwa na dakika ya kimya kuomboleza walioatharika kutokana na mashambulio ya bombu yaliyolenga majengo ya Umoja wa Mataifa  mjini Abuja, Nigeria.