Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa ya wasomali yawasili Yemen

Idadi kubwa ya wasomali yawasili Yemen

Zaidi ya Wasomali 3700 wamewasili Yemen wakibebwa na mashua kupitia Ghuba ya Aden. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kwamba hilo linajitokeza wakati wakimbizi wa ndani wanaendelea kupungua ndani mwa Somalia yenyewe, na idadi ya wakimbizi wanaoingia Kenya na Ethiopia pia imepungua.

Shirika hilo linasema kuwasili kwa Wasomali Yemen ni ushahidi wa vile wakimbizi wamekata tamaa na kuamua kukimbilia nchi ambayo yenyewe inakabiliwa na machafuko makali.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.