Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Irene chaanza kuleta madhara

Kimbunga Irene chaanza kuleta madhara

Shirika la Kimataifa linalohusika na upimaji wa hali ya hewa, limeonya juu ya uwezekano wa kutokea maafa zaidi wakati kunapojiri kimbunga Irene, ambacho tayari kimesababisha vifo vya watu 2 nchini Haiti na kusababisha uharibifu wa nyumba na mali nyingine ikiwemo bara bara.

Tayari watu 1,000 wameokolewa na kuwekwa kwenye vituo maalumu wakati kimbunga hicho kilipopiga kwenye eneo la pwani ya Caribbean juma hili. Kiwango cha tahadhari kimepandishwa zaidi nchini Haiti huku mashirika ya kimataifa yakiendelea kuchukua juhudi za ziada. Kuna taarifa za kutokea maafa ya hapa na pale katika nchi kadhaa zilizoko kwenye pwani ya Caribbean.