IOM yaendelea juhudi za kuwakwamua wahamiaji waliokwama Libya

26 Agosti 2011

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limetuma boti yake ya pili nchini Libya kwa ajili ya kuwakwamua wahamiaji waliokwama kwenye eneo hilo kufuatia mapigano ambayo sasa yamefikia kwenye kitovu cha kuangusha utawala wa Gaddafi. Boti hiyo imeanza kuondoka toka katika mji wa Benghazi ulioko kaskazini mwa Libya na kuelekea katika mji mkuu Tripoli.

Ndani yake imesheheni huduma mbalimbali ikiwemo madawa, huduma za dharura pamoja na mahitaji mengine muhimu. Zaidi ya wafanyakazi 50 wameambatana na boti hiyo kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu. Boti hiyo inatazamiwa kutia nanga mjini Tripoli mwishoni mwa juma hili

(JUMBE OMARI JUMBE NI MSEMAJI WA IOM)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud