Huduma za kitabibu ndiye kipaumbele chetu cha kwanza Libya: UM

26 Agosti 2011

Utoaji wa huduma za kibinadamu kama madawa, ni kipaumbele cha kwanza kinachozingatiwa nchini Libya. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa hivi sasa kunaandaliwa mpango mkakati wa siku 30 ambao utashughulikia mahitajio ya eneo hilo.

Afisa wa Umoja wa Mataifa Ian Martin ameuambia mkutano maalumu unaofanyika huko Uturuki kuwa, mashirika ya misaada ya kibinadamu yanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mpango mkakati wa kuisaidia Libya. Monica Morara ana taarifa kamili.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud