Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amekaribisha uchaguzi wa rais Cape Verde

26 Agosti 2011

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kurudiwa kwa uchaguzi wa rais katika nchi ya Cape Verde uliofanyika Jumapili iliyopita.

Ban amempongeza Jorge Carlos Fonseca kwa ushindi wa uchaguzi huo, ambao waangalizi wa kimataifa wamesema ulifanyika kwa njia ya amani na uaminifu. Pia amewapongeza watu wa Cape Verde kwa kupiga kura kwa utaratibu. Katibu Mkuu amesema ushiriakiano huu unaonyesha dhamira yao ya kuhifadhi na kuimarisha nchi yao ya muda mrefu, utamaduni na utawala wa demokrasia.

Ban ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kuendelea kusaidia watu na serikali ya Cape Verde katika jitihada zao za kukuza amani na maendeleo ya nchi yao na kanda ya Afrika Magharibi.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter