Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuumaliza mgogoro baina ya Israel na Palestina kumechelea sana:UM

Kuumaliza mgogoro baina ya Israel na Palestina kumechelea sana:UM

Kumaliza mgogoro baina ya Israel na Palestina na kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina kumechelewa sana. Hivyo ndivyo alivyosema mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Lynn Pascoe alipokuwa akitoa taarifa kwenye baraza la usalama kuhusu Mashariki ya Kati hii leo.

Bwana Pascoe amesema kwamba Waisrael na Wapalestina bado wako njia panda kuhusu majadiliano ya amani huku kutoaminiana kukiongezeka.