Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yakaribisha hatua ya Grenada kuwa mwanachama mpya wa mahakama hiyo

ICC yakaribisha hatua ya Grenada kuwa mwanachama mpya wa mahakama hiyo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imekaribisha hatua ya Grenada ambayo wiki hii imeridhia mkataba wa Roma unaotambua uwepo wa mahakama hiyo. Ikikaribisha hatua hiyo ICC imefanya tafriji maalumu mjini  Hague kama njia ya kupongeza uamuzi uliochukuliwa na Grenada kuridhia mkataba huo.

Kama ishara ya kukubalika kuwa mwanachama, rais wa mahakama hiyo Jaji Sang-Hyun Song alimkabidhi balozi wa Grenada hati maalumu inayoashiria kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa. Taifa la Grenada linakuwa taifa la 115 kuridhia kwa mkataba wa Rome ambao unatambua mahakama ya kimataifa.