Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban achagiza malengo matatu ya nishati kubadili uchumi wa dunia

Ban achagiza malengo matatu ya nishati kubadili uchumi wa dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia ambayo ni malengo ya nishati ili kubadili uchumi wa dunia na kufungua njia ya kuwa na mustakhabali bora, safi, salama na wenye matumaini.

Akizungumza kwenye mjadala maalumu

 kuhusu nishati endelevu kwa wote mjini Denver Colorado hapa Marekani, Ban amesema mambo hayo matatu muhimu kwanza ni kuhakikisha dunia nzima inapata huduma ya kisasa ya nishati, pili kuongeza uzalishaji wa nishati mara mbili na tatu kuongeza mara mbili kiwango cha kugawana nishati mbadala duniani.

Amesema mambo haya yatasaidia usawa, kufufua uchumi wa dunia na kusaidia kulinda uhusiano baina ya binadamu na mazingira ambayo yanatuwezesha kuishi. Amesema bila kutekeleza hayo taswira inayojitokeza kila mara wakati huu ni umasikini wa nishati na kutokuwepo usawa wa kugawana nishati hiyo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)