Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuanza kusambaza msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

WFP kuanza kusambaza msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linajiandaa kuanza kusambaza msaada wa chakula kwa mamia ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wanakabiliwa na hali ngumu baada ya kusitishiwa misaada. WFP pamoja na washirika wake inatazamiwa kutumia ndege ili kudondosha misaada ya chakula kwa wahitajio hao ambao ustawi wao unazidi kuzorota.

Familia zaidi ya 4,000 zilizoko katika kijiji cha Yida zinatazamiwa kufaidika na mpango huo. Eneo hilo lilisitishiwa kusambaziwa misaada ya kisamaria mwema kufuatia hali mbaya ya barabara iliyoharibika wakati wa msimu wa mvua.