UNESCO yalaani mauwaji ya mwandishi wa Pakistan

25 Agosti 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu, sayansi, na utamaduni ambalo pia linawajibika na utetezi wa uhuru wa vyombo vya habari UNESCO limelaani vikali mauwaji ya mwandishi wa habari wa Pakistan aliyeuwawa kwa kupigwa risasi wakati akirejea nyumbani. Mwandishi huyo wa habari Munir Shakar alipigwa risasi na watu wasiojulikana mnano Agosti 14 wakati akiwa njiani kurejea nyumbani akitokea kazini. Alikuwa akifanya kazi na kituo cha televesheni cha Sabzbagh .

Katika taarifa yake UNESCO mbali ya kulaani vitendo vya mauwaji kwa waandishi wa habari, lakini imeitaka dola ya Pakistan kuwafichua wahusika wa vitendo hivyo. UNESCO imesisitiza kuletwa kwenye mkondo wa sheria watekelezaji wa jinai hizo

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud