Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga Irene yaikumba Haiti:UM

Mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga Irene yaikumba Haiti:UM

Kimbunga Irene kimeleta mvua kubwa Kaskazini mwa Haiti na kusababisha mafuriko na kuharibu mashamba imesema ripoti rasmi ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kwamba maeneo 160 ya kuhifadhi watu yamefunguliwa endapo watahitaji hifadhi na misaada mingine.

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imesema hakuna maisha ya watu yaliyopotea hadi sasa wala uharibifu mkubwa kutokana na kimbunga Irene. OCHA imesema ni sehemu moja tu ya hifadhi ambayo imepokea watu 500, na baadhi ya barabara hazipitiki kutokana na maporomoko ya ardhi. Umoja wa Mataifa umeweka askari wake wa kulinda amani 12,000 tayari endapo watahitajika kwa operesheni za uokozi.

Haiti bado inajijenga upya kufuatia tetemeko la ardhi lililokatili maisha ya watu zaidi ya 200,000 mwaka 2010 na kuwaacha wengine milioni 2.3 bila makao. Nacho kimbunga Tomas Novemba mwaka jana kilizusha mafuriko makubwa na mlipuko wa kipindupindu uliathiri watu 20,000.