Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Sudan Kusini kurejesha utulivu kwenye eneo kulikozuka mapigano ya kikabila

Ban aitaka Sudan Kusini kurejesha utulivu kwenye eneo kulikozuka mapigano ya kikabila

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa mwito kwa serikali ya Sudan Kusini kurejesha hali ya utulivu katika jimbo la Jonglei ambalo limeshuhudia watu zaidi ya 600 wakifariki dunia kufuatia machafuko ya kikabila yaliyozuka wiki iliyopita. Taarifa nyingine zisizo rasmi zimesema kuwa katika machafuko hayo ambayo yalihusisha watu wa kabila la Murle na lile la Lou Nuer watu wengine 1,000 walijeruhiwa.

Akijadilia hali hiyo Ban amesitisha serikali ya Sudan Kusini kuchukua hatua zaidi ili kurejesha hali ya amani kwenye eneo hilo. Makundi hayo huzozana katika kile kinachoelezwa kama ugomvi wa mifugo.