Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UM ahutubia chuo kikuu cha Denver kuhusu maendeleo na nishati

Katibu Mkuu wa UM ahutubia chuo kikuu cha Denver kuhusu maendeleo na nishati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo yuko Denver Colorado hapa Marekani kutoa hotuba maalmu kwenye chuo kikuu cha Denver Josef Korbel kuhusu maendeleo na nishati .

Akiwa huko amekutana na wakuu wa eneo hilo na kuchagiza matumizi ya vyanzo ya nishati mbadala, pia amepokea tuzo ya kimataifa kutoka katika chuo hicho kwa kutambua juhudi zake za kuimarisha Umoja wa Mataifa , kuwawezesha wanawake na kupigia chepuo maendeleo endelevu.

Ban pia amekutana na viongozi wa makampuni mbalimbali ya nishati yakiwemo yanayohusika na nishati ya upepo, jua, na gesi asilia ili kujadili nishati endelevu kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea.