Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji ni muhimu kwa usalama wa chakula:FAO

Maji ni muhimu kwa usalama wa chakula:FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limesema maji ni muhimu sana katika kuhakikisha usalama wa chakula. Akizungumzia wiki ya maji mkurugenzi msaidizi wa mali asili wa FAO Alexander Meller amesema ni muhimu kutofautisha kilimo cha asili kinachotegemea mvua na kile cha umwagiliaji. Umwagiliaji unabadili kila kitu, unaongeza uzalishaji wakati wote bila kutegemea msimu wa muva. Akitoa mfano amesema matatizo ya njaa yanayoikabili pembe ya Afrika hivi sasa ni kutokana na hatari ya kilimo cha kutegemea mvua hasa yanapotokea mabadiliko ya hali ya hewa .

Ameongeza kuwa kilimo cha asili sio kibaya bali matatizo yanajitokeza pale mvua zisiponyesha na kusababisha ukame, hivyo umwagiliaji ni muhimu sana kwa uzalishaji wa chakula duniani. Amesema katika miaka 50 iliyopita idadi ya watu duniani imeongezeka mara mbili sawa na mahitaji ya chakula hivyo ni muhimu kutumia maji kuhakikisha usalama wa chakula.